Ufaransa: Ahadi hazitoshi kuokoa ulimwengu

Image caption Ufaransa: Ahadi hazitoshi kuokoa ulimwengu

Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema kuwa ahadi zinazotolewa na viongozi zinahitaji kutekelezwa ilikuokoa ulimwengu kutokana na mabadiliko ya tabia nchi

Hollande alikuwa akizungumza katika mkutano wa viongozi wa dunia mjini Paris

Viongozi hao wanaokutana mjini Paris, kwa kongamano la umoja wa mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, wameonya ,kuwa kuongezeka kwa viwango vya joto duniani ni janga la dharura.

Viongozi hao wameahidi kupunguza uzalishaji wa hewa chafu ya mkaa inayosababisha viwango hivyo vya joto kuongezeka.

Lakini mwandishi wa BBC mjini Paris amesema bado kuna na changamoto nyingi.

Haki miliki ya picha epa
Image caption Wajumbe wana siku kumi na mbili kuafikiana kuhusu jinsi ya kupunguza viwango vya joto kwa asilimia 2%

Haijabainika ni vipi mataifa yatafadhili mkataba utakaoafikiwa au jinsi mkataba huo utakavyotekelezwa.

Wajumbe wana siku kumi na mbili kuafikiana kuhusu jinsi ya kupunguza viwango vya joto kwa asilimia 2% .

Lakini wanaharakati wa mazingira wanasema viwango vilivyopendekeza havitoshi kuzuia tatizo hilo.