Iran yakana uhusiano na magaidi

Image caption Raia wa Iran

Serikali ya Iran imekana kuwa na uhusiano wowote na wanaume wawili waliokamatwa wakikisiwa kupanga mashambulizi ya kigaidi dhidi ya maeneo yanayomilikiwa na mataifa ya magharibi nchini Kenya.

Balozi wa Iran nchini Kenya Hadi Farajvad, anasema kuwa licha ya kuwepo uwezekano kuwa wanaume hao walizuru Iran, hakuna aliye na uhusiano na mashirika ya usalama ya nchi hiyo.

Siku ya Jumamosi taarifa kutoka kwa wizara ya mambo ya ndani nchini kenya, ilisema kuwa wanaume hao walikiri kuwa walikuwa na njama ya kupanga mashambulizi ya kigaidi dhidi ya maeneo yanayomilikiwa na mataifa ya magharibi nchini Kenya, na walikuwa na uhusiano na kikosi cha kijeshi kinachofahamika kama Quds Force nchini Iran.