Nigeria yamkamata afisa aliyeiba pesa

Dasuki Haki miliki ya picha AP
Image caption Dasuki alikuwa mshauri wa Rais mstaafu Goodluck Jonathan

Wakuu nchini Nigeria wamemkamata afisa wa ngazi ya juu wa zamani anayeshtumiwa kwa wizi wa dola bilioni mbili ambazo zilinuiwa kununua silaha za kupambana na wanamgambo wa Boko Haram.

Sambo Dasuki alikuwa mshauri wa Usalama katika serikali ya Rais aliyestaafu Goodluck Jonathan.

Anadaiwa kutoa kandarasi ghushi za ununuzi wa helikopta kumi na mbili, ndege nne na silaha nyingine. Amekanusha madai hayo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wakati wa kampeni Rais Buhari aliahidi kukabiliana na ufisadi

Maafisa wa ngazi za juu wamekuwa wakikamatwa nchini Nigera kujibu madai ya ufisadi tangu rais wa sasa Muhammadu Buhari kushika hatamu za uongozi na kuahidi kuwa hatavumilia ufisadi.