Bunge la Uingereza kupiga kura leo

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bunge la Uingereza kupiga kura leo

Bunge la uingeraza linatarajiwa kupiga kura hii leo kuunga mkono kampeni ya Uingereza dhidi ya wapiganaji wa Islamic State nchini Syria na Iraq.

Muda wa takriban saa kumi unusu umetengwa kwa mjadala bungeni. Wabunge wanatarajiwa kuuliza kuhusu madhara yapi yatakayotokana na mashambulizi nchini syria, yatafutiwa kwa njia ipi na vikosi vya nchi kavu na ikiwa uingereza ina mikakati yoyote.

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Lebour Jeremy Corbyn anapinga mipango hiyo lakini anaruhusu wanachama wake kuiunga mkono serikali ikiwa watataka hivyo.

Ndege za kivita za Uingereza zilizo nchini Cyprus huenda zikajiunga na mashambulizi ya nchi za magharibi ikiwa bunge litatoa idhini.