Uchina kujenga bunge mpya Zimbabwe

Rais wa China
Image caption Rais wa China Xi Jinping

Uchina imeahidi kujenga miradi mipya nchini Zimbabwe ikiwemo majengo ya bunge na mtambo mpya wa kawi ya mvuke.

Mradi huu utajengwa katika eneo Hwange magharibi mwa nchi.

Haki miliki ya picha AP
Image caption China ni mshirika wa karibu wa Zimbabwe

Tangazo hili limetolewa wakati Rais wa China Xi Jinping akifanya ziara ya siku mbili nchini Zimbabwe.

Hii ndio ziara ya kwanza kwa kiongozi wa China kufanya nchini Zimbabwe kwa karibu miongo miwili.