NATO yaialika Montenegro kujiunga nayo

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption NATO yaialika Montenegro kujiunga nayo

Shirika la kujihami la mataifa ya Ulaya NATO limealika Montenegro kujiunga nalo kama mwanachama wake wa 29.

Hatua hiyo imechukuliwa miaka 16 baada ya NATO kurusha mabomu nchini Montenegro wakati wa vita vya Kosovo.

Wakati huo Montenegro ilikuwa moja ya mataifa ya Yugoslavia.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg, ameipongeza Montenegro

Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg, ameipongeza Montenegro akisema huo ni mwanzo wa ushirikiano mpya.

Urusi haijaridhishwa na hatua hiyo na imesema kuendelea kupanua shirika la NATO kutakuwa na athari .