Thailand yahofia magaidi kutoka Syria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Polisi nchini Thailand

Polisi nchini Thailand wanachunguza ripoti kuwa wanamgambo kumi kutoka kundi la wapiganaji wa Islamic State wameingia nchini humo na wanapanga kushambulia sehemu zinazomilikiwa na Urusi.

Shirika la habari nchini Urusi la FSB linaamini kuwa kundi hilo limesafiri kutoka nchini Syria.

Sita kati yao wanaripotiwa kuelekea maeneo ya kifahari ya Pattaya na Phuket huku wengine wakiwa hawajulikani waliko.

Polisi nchini Thailand wanasema kwa hawajafanikiwa kuthibitisha uwepo wa raia hao wa Syria. Zaidi ya watu milioni moja unusu raia wa Urusi walizuru Thailand mwaka 2013.