'Walioua 14 Marekani wangeua mamia'

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ndugu wakifarijiana kufuatia mauaji huko San Bernadino Marekani

Shirika la kijasusi la Marekani FBI limegundua kuwa waliohusika katika shambulio jana la kuua watu 14 nchini Marekani walikuwa ni wanandoa mke na mume.

Limesema wanandoa hao Syed na Farook na mke wake Tashfeen Malik ambao wote waliuawa walikuwa na silaha za kutosha na mabomu ya kuua mamia ya watu.

FBI imesema sababu ya wanandoa hao kufanya mashambulizi hayo hajifahamika lakini pia limegundua kuwa Farook alikuwa akifanya mawasiliano na wapiganajiwa wa Islamic State kwa kutumia mitandao ya kijamii.

Mkurugenzi wa Shirika la kijasusi FBI Los Angeles David Bowdich amesema ni mapema kusema nini kilichowasukuma kufanya mauaji hayo.

"Ukifuatilia mipango ya awali iliyokuwa ikiendelea, kiwango cha silaha alichokuwa nacho, idadi ya silaha na zana nyingine ni wazi kabisa kulikuwa na mipango hapa ndicho tunachokijua. Hatujui kwanini, hatujui kama hii lilikuwa ni lengo lao au kama kuna kitu kingine kilchowasukuma kufanya jambo hili, kwa kweli hatujui."

Wakati hayo yakiendelea ibada kwa ajili ya kuwakumbuka wote waliokufa katika shambulizi hilo ilikuwa inaendelea.