Morgan Freeman anusurika ajali ya ndege

Haki miliki ya picha AP
Image caption Msanii mkongwe Morgan Freeman alinusurika katika ajali ya ndege mjini Mississippi Marekani.

Msanii mkongwe Morgan Freeman alinusurika katika ajali ya ndege mjini Mississippi Marekani.

Duru zinaarifu kuwa mshindi huyo wa tuzo ya Oscar pamoja na rubani wake walinusurika kufariki baada ya ndege waliokuwa wakisafiria kupasuka gurudumu lake ilipokuwa ikikwenda kwa kasi kabla ya kupaa angani.

Ndege hiyo ya kibinafsi ililazimika kutua mjini Tunica takriban kilomita 65 kutoka Clarksdale, Mississippi ilikopoteza mwelekeo na kwenda nje ya barabra maalum ya kutua.

Katika taarifa aliyotuma kwa vyombo vya habari, Nyota huyo nguli wa ''The Shawshank Redemption ''alisema

''wakati mwengine mambo huenda mrama kwa hivyo kilichotokea leo ilikuwa mlipuko wa gurudumu ambayo ilisababisha hitilafu zaidi''

Hata hivyo namshukuru rubani wangu Jimmy Hobson tulitua salama wa salmin.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Alituzwa mwaka wa 2005 kwa mchango wake katika filamu ya 'Million Dollar Baby'.

"Ndege bila shaka iliharibika hata hivyo nashukuru kwa wale walioniombea mimi ni mzima wa afya'' alisema bwana Freeman .

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 78 amewahi kuteuliwa kwa vitengo 7 vya tuzo za Oscar katika filamu alizoigiza Driving Miss Daisy, Street Smart na Invictus.

Alituzwa mwaka wa 2005 kwa mchango wake katika filamu ya 'Million Dollar Baby'.