Gavana wa Aden ameuawa katika shambulizi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Gavana wa mji wa Aden nchini Yemen Jaafar Mohamed Saad ameuawa

Maafisa wa kiusalama nchini Yemen, wanasema kuwa mlipuko mmoja mkubwa umemuua gavana wa mji wa Aden ulioko bandarini mwa taifa hilo pamoja na walinzi wake.

Wanasema kuwa gavana, Jaafar Mohamed Saad, alikuwa akielekea afisini kwake wakati msafara wake uliposhambuliwa ghafla.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Duru zinasema kuwa mlipuko huo ulisababishwa guruneti iliyorushwa kwa mzinga.

Duru zinasema kuwa mlipuko huo ulisababishwa guruneti iliyorushwa kwa mzinga.

Jenerali Saad alikuwa mhusika mkuu na kiongozi kundi wa wapiganaji wanaounga mkono serikali iliyowatimua waasi wa kishia wa-Houthi kutoka mji wa Aden mapema mwaka huu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Makao makuu ya serikali ya Aden iliposhambuliwa

Aliteuliwa gavana mwezi Oktoba mwaka jana.

Taarifa za hivi punde zinasema kuwa kundi la Islamic State limekiri kuhusika katika shambulizi hilo.