Mmarekani aliyejiunga na al-Shabab akamatwa

Garissa Haki miliki ya picha AP
Image caption Mmarekani huyo amekiri kuhusika shambulio la Garissa lililoua watu 148

Raia wa Marekani ambaye alijiunga na kundi la wapiganaji wa Kiislamu wa al-Shabaab nchini Somalia amekamatwa.

Afisa wa serikali ya Somalia ameambia BBC kwamba Mwamerika huyo alikamatwa na wanajeshi kusini magharibi mwa Mogadishu akiwatoroka wapiganaji pinzani wa Kiislamu.

Hii ni baada ya wenzake kuuawa kwenye vita vya kambi pinzani ndani ya kundi hilo.

Mkuu wa wilaya ya Barawe Hussein Barre Mohamed amesema ingawa mwanamume huyo amekuwa Somalia wka muda mrefu, hakuweza kuzungumza Kisomali.

Kundi la Al-Shabab huegemea mtandao wa al-Qaeda, lakini baadhi ya makundi yamehama na kujiunga na kundi linalojiita Islamic State.