Syria yasema mauaji ya wanajeshi ni uchokozi

Syria Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Syria imekasirishwa na mashambulio ya angani yanayotekelezwa nchini humo na vikosi vya nchi za Magharibi

Serikali ya Syria imesema shambulio ambalo limedaiwa kutekelezwa na wanajeshi wa muungano unaoongozwa na Marekani, na ambalo lilisababisha vifo vya wanajeshi watatu wa Syria, ni uchokozi.

Damascus imelitaka Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuingilia kati kuzuia kujirudia kwa kisa kama hicho.

Muungano unaoongozwa na Marekani umekanusha kushambulia kambi ya jeshi mkoa wa Deir al-Zor mashariki mwa Syria.

Majeshi ya serikali yanadhibiti sehemu ya mkoa huo, sehemu nyingine zikidhibitiwa na wapiganaji wanaojiita Islamic State.

Viongozi wa wamekuwa wakihimiza majeshi yanayoshambulia wapiganaji Syria kushirikiana na kuratibu mashambulio kwa pamoja.