Treni yarejea Kampala mara ya kwanza tangu 1998

Image caption Treni yarejea Kampala mara ya kwanza tangu 1998

Huduma ya gari moshi ya kubeba abiria imerejea mjini Kampala Uganda kwa mara ya kwanza tangu 1998

Gari moshi hilo lenye mabehewa 5 litakuwa linahudumu kutoka katikati ya mji mkuu wa Kampala na kwenda takriban kilomita 14 nje ya mji huo.

Watu wachache waliojua kuhusu kurejea kwa huduma hiyo walifika katika kituo cha gari moshi cha Kampala.

Safari hiyo inapitia katika vitongoji vya mji huo ambao kwa sasa haipitiki kwa sababu ya mijengo mingi.

Image caption Gari moshi hilo lenye mabehewa 5 litakuwa linahudumu kutoka katikati ya mji mkuu wa Kampala na kwenda takriban kilomita 14 nje ya mji huo.

Mtangazaji wa BBC aliyeabiri gari moshi hilo aliona vijiji vilivyoko karibu na reli ambapo aliwaona wanawake wakipika kiamsha kinywa na pia taswira nzuri ya uwanja mkuu wa taifa ulioko Nambole.

Japo huduma hiyo ni mpya gari moshi lenyewe ni nzee mno na hata rangi mpya iliyopakwa kwenye mabehewa hayo matano yanayotumika haijakauuka vyema.

Safari ya mkondo mmoja inagharimu senti 45 kwa dola.

Image caption Safari ya mkondo mmoja inagharimu senti 45 kwa dola.

Reli nchini Uganda ilijengwa miaka ya mwanzomwanzo ya 1900 na wakoloni kutoka Uingereza.

Wakati huo reli hiyo ilikuwa na dhumuni kuu ya kubeba mali ghafi kuipeleka katika bandari ya Mombasa nchini Kenya na kisha kusafirishwa kwa meli hadi Uingereza.

Muundo msingi wa reli hiyo haujaboreshwa kwa kiasi kikubwa mbali na kusafisha tu haswa baada ya mgogoro wa kisiasa uliopelekea kuvunjika kwa muungano wa Afrika Mashariki miaka ya 1970