Ushindi mkubwa kwa upinzani Venezuela

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ushindi mkuwa kwa upinzani Venezuela

Chama cha upinzani nchini Venezuela kumeshinda wingi wa viti bungeni kwa mara ya kwanza tangu chama cha kisoshiolisti kiingie madarakani 1999 chini ya uongozi wa rais wa zamani Hugo Chavez .

Rais wa baraza kuu la uchaguzi Tibisay Lucena, amesema kuwa upinzani umeshinda takriban viti 99 kati ya viti 167.

Matokeo ya awali ya ubunge

Venezuela

  • 99 Muungano wa Upinzani Mesa de Unidad Demócratica

  • 46 Chama tawala PSUV

  • 22 Matokeo ambayo hayajatangazwa

  • 12 Idadi ya viti ambavyo upinzani unahitaji kudhiti thuluthi mbili ya bunge la Venezuela' lenye viti 167

AP

Chama cha kisosholisti cha rais Nicholas Maduro kilipata viti 46.

Fataki zilisikika katika wilaya zilizo na wafuasi wa upinzani katika mji mkuu Caracas kufutia kutangazwa kwa matokeo hayo.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mapema ghasia zilizuka kwenye baadhi ya vituo vya kupigia kura huku wanachama wa upinzani wakilalamikia kuwepo udanganyifu

Mapema ghasia zilizuka kwenye baadhi ya vituo vya kupigia kura huku wanachama wa upinzani wakilalamikia kuwepo udanganyifu baada ya tume ya uchaguzi kuongeza muda wa kupiga kura kwa saa moja zaidi.

Japo rais Maduro mwenyewe hakuwa anawania kiti chochote, amekubali kushindwa na na kutaja matokeo hayo kuwa ''matokeo mabaya zaidi''

Kulingana na Maduro amelaumu kushindwa huko kumetokana na ''vita vya kiuchumi '' kutoka kwa vyama vya upinzani dhidi ya serikali yake.

Uchumi wa Venezuela ulivyodorora

100%+

Mfumuko wa bei mwaka huu 2015

  • -10% Zao la taifa 2015

  • -6% Miradi mipya 2016

  • 18.1% Ukosefu wa ajira 2016

Reuters

''kwa kweli tumenyenyekea na kukubali matokeo haya ya uchaguzi wa kidemokrasia nchini Venezuela na ninachowza kusema ni kuwa huu ni ushindi kwa watu wa Venezuela na demokrasia''.

"hata hivyo tumeshindwa leo, sasa tunaanza kujenga jamii yenye umoja huu ndio mwanzo tu '' alisema bwana Mana Maduro.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kiongozi wa upinzani bwana Jesus Torrealba amesema ''watu wa venezuela walikuwa wanataka mabadiliko na bila shaka wamepiga kura na sauti yao imesikika.

Kiongozi wa upinzani Henrique Capriles aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa twitter ''matokeo haya ni kama tulivyotarajia. Bila shaka hakuna mabadiliko''.

Mwenzake bwana Jesus Torrealba amesema ''watu wa venezuela walikuwa wanataka mabadiliko na bila shaka wamepiga kura na sauti yao imesikika.