Papa Francis kuzindua mwaka wa huruma

Kanisa
Image caption Mamilioni ya mahujaji wanatarajiwa kutembelea Vatican

Kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Francis, leo ataanzisha rasmi mwaka wa Kikatoliki wa kuadhimisha unyenyekevu na huruma.

Kanisha Katoliki limeadhimisha maswala mbalimbali kwa zaidi ya miaka 700 iliyopita. Maadhimisho ya mwisho ya mwaka kama huu yalifanywa mwaka 2000.

Ili kutilia mkazo mada ya mwaka huu wa huruma, Papa Francis amesema kuwa kwa miezi 12 ijayo mapadri wote watawapa msamaha wanawake walioavya mimba wanaoomba msamaha.

Kanisa Katoliki linafunza kuwa utoaji mimba ni kosa linaloweza kufanya mtu kufukuzwa Kanisani.

Mwaka wa Maadhimisho unaanza rasmi kwa kuufungua mlango maalumu wa St Peter's Basilica ambao huzibwa kwa matofali miaka ambayo si ya maadhimisho.

Mamilioni ya mahujaji wanatazamiwa kutembelea makao hayo makuu ya Kanisa Katoliki ya Vatican kuadhimisha mwezi huu muhimu wa kalenda ya Kanisa.