Ukungu:Viwanda na shule zafungwa China

Haki miliki ya picha AFP Getty
Image caption Ukungu:Viwanda na shule zafungwa China

Vikwazo vigumu vimewekea mjini Beijing ili kupunguza uchafuzi wa hewa baada ya mji huo mkuu wa China kutangaza tahadhari kwa mara ya kwanza kabisa.

Nusu ya magari ya mji huo yamepigwa marufuku ya kuingia barabarani.

Shule zimefungwa huku viwanda vingi na majengo yakifungwa.

Beijing umefunikwa na ukungu unaotokana na hewa mkaa.

Katika mji mkuu wa Beijing imekuwa vigumu kuona zaidi ya mita 100.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Shule zimefungwa huku viwanda vingi na majengo yakifungwa.

Makataa haya yanatarajiwa kudumu hadi siku ya Alhamisi.

Viwango vya kemikali hewani ni mara kumi zaidi kuliko vile vinavyotajwa kuwa salama kwa afya ya binadamu na shirika la afya duniani WHO.