FBI: Washambuliaji San Bernardino walijiandaa

Malik na Farook Haki miliki ya picha ABC NEWS AP
Image caption Malik pamoja na Farook watu waliotekeleza mashambulizi ya San Bernardino

Watu wawili waliopanga mashambulizi ya San Bernardino yaliyowauwa watu 14 walifanya mazoezi ya shambulio hilo siku kadhaa kabla ya kulifanya, shirika la ujasusi la FBI limesema.

Tashfeen Malik na mumewe Syed Farook walitembelea eneo hilo lililopo Los Angeles, alisema David Bowdich, naibu mkurugenzi wa assistant director of FBI' ofisi ya Los Angeles.

Alisema wote walipata mafunzo ya itikadi kali na wamekuwa na itikadi hizo ''kwa muda''

Haki miliki ya picha getty images
Image caption Hakuna ushahidi ikiwa mashambulizi ya San Bernardino yalipangwa nje ya nchi

Marekani inachunguza shambulio hilo la wiki iliopita , lililotokea kwenye kituo cha afya , kama kitendo cha ugaidi.

Lakini Bwana Bowdich amesema bado hawajapata ushahidi wowote kwamba mkasa huo wa wiki jana , ambao ni mkubwa wa kigaidi tangu shambulizi la 9/11, ulipangwa nje ya nchi.

Washambuliaji wote wawili waliuawa wakati polisi walipowafyatulia risasi.