Mahakimu 20 wafutwa Ghana kwa sababu ya rushwa

Anas
Image caption Mwanahabari huyo mfichuzi alinakili visa vya ulaji rushwa kwa miaka miwili

Mamlaka ya mahakama nchini Ghana imewafuta kazi mahakimu 20 ambao wamehusishwa na sakata la kupokea rushwa.

Waliotimuliwa ni mahakimu wa mahakama za chini na bado kuna baadhi ya mahakimu wa mahakama kuu ambao wamesimamishwa kazi huku uchunguzi zaidi ukiendelea.

Ufisadi huo ulibainika baada ya mwandishi wa habari za uchunguzi, Aremeyaw Anas, alipokusanya kwa muda wa miaka miwili kanda za video za masaa yapatayo 500 kama ushahidi dhidi ya zaidi ya mahakimu 30 na takriban watumizi wa mahakama wapatao mia mbili.

Kutokana na sakata hilo, baadhi nchini Ghana wanataka kuwepo kwa mabadiliko katika mahakama nchini humo.