Wafugaji washtakiwa kwa kuua simba 2 Kenya

Haki miliki ya picha XINHUA
Image caption Wafugaji washtakiwa kwa kuua simba 2 Kenya

Wafugaji wawili wa mifugo wamefikishwa mahakamani nchi Kenya.

Wanatuhumiwa kwa kuweka sumu kwenye mzoga wa ng'ombe ambao wafugaji hao wanadai kundi la simba liliwavamia na kuwaua.

Kundi la simba hao wanane linalofahamika kama The Marsh Pride lilionekana mwisho karibu na hoteli ya kifahari ya Governors Camp.

Wawili hao, Simindei Naururi na Kulangash Toposat wanakabiliwa na mashtaka ya kuua kwa kukusudia simba hao ambao ni rasli mali ya taifa.

Simba wanane wamegonjeka.

Simba hao ni maarufu baada yao kuonyeshwa katika makala ya wanyama pori ya runinga ya BBC ya Big Cat Diary.

Image caption Vifo hivyo ni kilele cha mzozo kati ya jamii ya wafugaji wa kuhama hama ya wa-Maasai ambao wanalazimika kuchunga mifugo wao ndani ya mbuga ya wanyama ya Maasai Mara

Vifo hivyo ni kilele cha mzozo kati ya jamii ya wafugaji wa kuhama hama ya wa-Maasai ambao wanalazimika kuchunga mifugo wao ndani ya mbuga ya wanyama ya Maasai Mara

Shirika la huduma ya wanyama pori nchini Kenya KWS limeonya huenda simba zaidi walikula mzoga huo wa ng'ombe uliowekwa sumu.

Wafugaji hao wanadai kuwa walivamiwa na kundi la Simba ambao waliua mifugo watatu.

Tukio hilo lilitokea jumamosi tarehe 5.Kufikia Jana simba wawili walikuwa wameaga dunia tayari.