UN yawatetea wakimbizi wa Syria

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wakimbizi wa Syria

Umoja wa mataifa umetoa wito kwa serikali ya Jordan kuwaruhusu idadi ya wakimbizi wanaokadiriwa kufikia elfu kumi na mbili wa Syria ambao wamekwama katika mpaka wake wakiwa wamedhoofika vibaya.

Umoja wa mataifa umesema idadi ya wakimbizi wanaotaka kuingia Jordan imekuwa ikiongezeka kwa kasi katika wiki za hivi karibuni, ikujumuisha watoto kadhaa,watu wazima na wagonjwa.

Mwandishi wa BBC aliyeko nchini Jordan anasema kwamba nchi hiyo imefunga njia zote za panya zinazotoa mwanya wa watu kuingia nchini humo kiholela,takriban miezi nane iliyopita na wakimbizi walio wengi wameondoka nchini humo .

Hata hivyo umoja wa mataifa unakadiria kuwa Jordan bado ina idadi ya wakimbizi wapatao laki sita wa Syria.kikundi cha kinachoendesha kampeni cha kutetea haki za binaadamu kimeishutumu Jordan kwa kuhatarisha uhai kwa kuzuia wakimbizi wapya kuingia nchini mwake.