Serikali yafikia mkataba na waasi Syria

Mji wa Horms Haki miliki ya picha AP
Image caption Mji wa Horms sasa mikononi mwa serikali

Katika mji wa Syria wa Horms, makubaliano ya ndani ya usitishaji mapigano yamefikia kuruhusu mamia ya wapiganaji kuondoka maeneo ya mwisho yanayodhibitiwa na upinzani.

Makubaliano hayo katika mji wa Al Waer yanamaanisha kuwa mji wa tatu kwa ukubwa wa Syria sasa umerejea mikononi mwa serikali baada ya miaka kadhaa ya ghasia .

Wanaharakati wa Syrian wakati mmoja waliuita mji wa Homs "mji mkuu wa mabadiliko''

Mkataba huu muhimu umefikiwa baada ya mazungumzo yaliyoahirishwa mara kwa mara ya miaka miwili.

Image caption Mamia ya wapiganaji watasafirishwa chini ya ulinzi mkali kuelekea eneo la Idlib

Chini ya awamu ya kwanza ya mkataba huo, mamia ya wapiganaji, wakiwemo wenye uhusiano na kundi la Al-Qaeda, wataondoka katika maeneo jirani ya vita.

Watasafiri chini ya ulinzi mkali kuelekea eneo la kaskazini la Idlib linalodhibitiwa na waasi.

Makundi zaidi yenye itikadi za wastani ambayo yamekubali usitishaji mapigano yatabakia katika mji wa Al Waer kwa muda.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Serikali ya Syria imeyataja makubaliano na makundi ya wapiganaji kama mafanikio makubwa

Makubaliano haya ya usitishaji mapigano yaliyoungwa mkono na Umoja wa Mataifa yamewezesha misururu ya kwanza ya misaada ya chakula kuingia katika mji wa Al Waer kwa mara ya kwanza katika kipindi cha karibu mwaka mmoja.

Serikali ya Syria, ambayo imekamilisha mikataba sawa na hiyo katika maeneo mengine , inauangalia mkataba huu kama njia bora zaidi ya kumaliza mapigano kulingana na masharti yake. Katika baadhi ya maeneo wameruhusu baadhi ya makundi kubaki na silaha zake na mengine yameachiwa udhibiti wa jamii zao