Watu 50 wauawa Kandahar

wapiganaji wa Taleban
Image caption Waoiganaji wa Taliban kumi na mmoja waliawa

Serikali ya Afghanstan inasema vikosi vyake vimeua wapiganaji katika kundi la mwisho la Taliban walioshambulia uwanja wa ndege wa Kandahar.

Watu hamsini wamefariki katika mapigano hayo yaliyodumu kwa zaidi ya saa ishirini na nne, wengi wao wakiwa ni raia.

Wapiganaji wa Taleban kumi na mmoja waliuawa.

Image caption Baadhi ya wapiganaji wa Taleban wa Afghanstan

Mashambulizi ya Taleban katika moja ya ngome kubwa nchini Afghanstan yamefanyika huku mkutano wa kikanda wa amani ukiendelea katika mji mkuu Islamabad, ambako rais, Ashraf Ghani, aliiomba Pakistan kusaidia mazungumzo ya kufikiwa kwa mazungumzo ya amani.

Mapigano hayo yalianzia kwenye uwanja wa ndege wa Kandahar hapo jana na Taliban wanasema wanamgambo wake kadhaa waliweza kuingia kwenye uwanja huo na kulipua mabomu ya kujitolea muhanga.

Katika kauli yake wizara ya ulinzi ya Afghanstan amesema raia thelathini na saba wameuawa, huku madaktari wakiripoti kuwa wengi miongoni mwa waliouawa ni wanawake na watoto.