Adele atawala tuzo za BBC

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Adele

Nyota wa muziki wa Pop Adele ametawala tuzo za pili za BBC baada ya kushinda tuzo ya msanii bora Uingereza na maonyesho bora ya moja kwa moja.

Mwanamuziki huyo hakuweza kuhudhuria sherehe hiyo,lakini alituma ujumbe unaosema nimefurahi sana, nilitoa muziki wangu mpya hivi karibuni.

Mwanamuziki wa Ireland Hozier alishinda tuzo ya wimbo bora wa mwaka 'Take me to Church'.

Taylor Swift pia alishinda tuzo ya msanii bora wa kimataifa huku akikubali tuzo hiyo kupitia video akiwa nchini Australia.

''Mungu wangu tuzo hii ni nzito sana.nafurahi sana kwa kunitumia kwa sababu lazima imewagharimu''.