Mauzo ya hisa yayumba Uchina

Guo Guangchang Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Guo Guangchang mmiliki wa kampuni ya Fuson International

Mauzo ya kampuni kubwa binafsi ya uwekezaji ya katika soko la hisa la Mjini Hong kong Uchina yamesimamishwa kwa muda. Hii ni inafuatia hali ya wasi wasi kuhusu alipo mwenyekiti wa kampuni hiyo Guo Guangchang huku ripoti moja ikisema kuwa hajaweza kupatikana tangu Alhamis Mchana .

Fosun anamiliki mapuni ya bima, makazi na maduka ya jumla.

Anamiliki kampuni ya utalii ya ufaransa ijulikanayo kama Club Med.

Guo Guangchang ni mmoja wa matajiri wakubwa nchini Uchina.

Haki miliki ya picha
Image caption Mauzo ya hisa ya kampuni ya Fosun International yapungua katika soko la hisa la Hong kong

Mtandao wa Caixin ulinukuu chanzo kimoja cha habari kikisema wafanyakazi wa Fosun walishindwa kuwasiliana na Bwana Guo.

Aidha ulinukuu ujumbe uliotumwa kweney mitandao ya kijamii zikisema mara ya mwisho alionekana akiwa na polisi mjini Shanghai.

Fosun International,kampuni ambayo ilianzisha kampuni ya Shanghai Fosun Group, ilisajiriwa Hong Kong mwaka 2007.

Katika taarifa ya soko la hisa la Hong Kong iliyotolewa Ijumaa ,kampuni hiyo ilisema kuwa kiwango chake cha hisa kitaathirika kuanzia saa tatu za asubuhi.