Kunenepa ni tishio la kiafya kwa wanawake UK

Image caption Wanawake walionenepa Uingereza

Kunenepa kupitia kiasi ni tishio kubwa kwa afya ya wanawake pamoja na ile ya vizazi vijavyo ,ameonya Afisa mkuu wa matibabu nchini Uingereza Dame Sally Davies.

Katika ripoti yake ya kila mwaka inayowalenga wanawake,amesema kuwa kukabiliana na tatizo hilo kunafaa kupewa kipaumbele kitaifa ili kuzuia janga la kiafya.

Amesema kuwa kampuni za chakula zinafaa kuchukua hatua la sivyo zitozwe kodi ya sukari.

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Mwanamke aliyenenepa

Dame Sally pia anataka tiba mwafaka ya saratani ya mayai ya uzazi miongoni mwa wanawake pamoja na majadiliano zaidi na udhaifu.

Daktari huyo amesema kuwa kunenepa kupitia kiasi ni swala nyeti na linafaa kupewa kipaumbele na watu wote na hususan wanawake kwa kuwa hupunguza miaka yao ya kuishi.

Nchini Uingereza mwaka 2013,asilimia 64 ya wanawake walio kati ya umri wa miaka 34-44 na asilimia 71 ya wanawake walio na umri kati ya 45-54 walitajwa kuwa wanene kupitia kiasi.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kunenepa

Kunenepa kunaongeza hatari za kupatikana na magonjwa mengi ikiwemo saratani ya matiti,ugonjwa wa sukari wa aina ya pili pamoja na ule wa moyo.

Dame Sally ameonya kwamba iwapo sekta ya chakula haitasitisha tatizo hilo basi kodi mpya dhidi ya bidhaa za sukari huenda ikawa suluhu.