Mugabe: Acheni kugombania kiti changu

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais Robert Mugabe

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amewataka wanasiasa kukoma mara moja kugombania kuhusu nani atamarithi.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 91, amesema hayo katika kongamano la kila mwaka la chama tawala- Zanu-PF huko Victoria Falls.

Pia amevishutumu vikosi vya jeshi, Polisi na idara ya ujasusi kwa kuungana na wanaopigania wadhfa wa urais huku wakijadiliana kuhusu ni nani atakayechukua mahala pake.

Bw Mugabe amesema kuwa hakuna mabadiliko katika uongozi wa taifa hilo.

Waandishi habari wanasema kuwa, kumekuwa na tetesi kuwa mkewe, Grace Mugabe, huenda akapandishwa cheo na kuwa makamu wa Rais.