Mkurugenzi wa Yahoo ajifungua pacha

Marissa Nayer Haki miliki ya picha GETTY IMAGES
Image caption Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Yahoo Marissa Mayer anasema atachukua muda mfupi wa likizo ya uzazi

Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya teknolojia ya Yahoo, Marissa Mayer, amejifungua watoto pacha wa kike mapema Alhamis.

Katika ujumbe alioutuma kwenye ukurasa wake wa tumbir Bi Mayer aliandika: "Zack na mimi tunapenda kutangaza kwamba watoto wetu pacha wa kike wanaofanana wamezaliwa!" na kuongeza kuwa "familia yetu yote inaendelea vema!".

Anatarajia kuchukua "muda mfupi" wa likizo ya uzazi.

Yahoo ilitangaza Jumatano mpango wa kuhamishia sehemu ya biashara yake ya mtandao kwa kampuni tofauti.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kampuni ya yahoo hutoa likizo rasmi ya uzazi ya wiki 16

Bi Mayer na mumewe Zachary Bogue wana mtoto mvulana mwenye umri wa maika mitatu aitwaye Macallister.

Baada ya kuzaliwa kwake Bi Mayer alipumzika kwa wiki mbili tu, suala ambalo lilizua hisia kali wengi wakimkosoa kuwa anaonyesha mfano mbaya kwa wafanyakazi akina mama katika kampuni ya Yahoo.

Kampuni ya Yahoo hutoa likizo rasmi ya uzazi ya wiki 16 kwa akina mama waliojifungua