MSF sasa yasema watu 42 waliuawa Kunduz

MSF Haki miliki ya picha AFP
Image caption Awali, MSF ilisema watu zaidi ya 30 walifariki

Shirika la madaktari wasio na mipaka (MSF) limesema watu waliouawa kwenye shambulio lililotekelezwa na Marekani kwenye hospitali yake Afhanistan Oktoba imeongezeka hadi 42.

Kupitia taarifa, shirika hilo limesema limebadilisha idadi ya waliofariki baada ya kufanywa kwa uchunguzi zaidi.

Awali, MSF walikuwa wameripoti kuwa watu zaidi ya 30 walifariki.

Kwa mujibu wa shirika hilo, takwimu sahihi zinaonyesha wafanyakazi 14 wa MSF walifariki pamoja na wagonjwa 24 na watu wanne wa kuwatunza wagonjwa.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Marekani ilisema shambulio hilo lilitekelezwa kimakosa

Hospitali hiyo iliyoko Kunduz iliangushiwa mabomu wakati wa mapigano kati ya vikosi vya usalama na wapiganaji wa Taliban.

Uchunguzi tofauti uliofanywa na Marekani ulisema shambulio hilo lilitokana na kosa la kibinadamu, kufeli kwa mifumo na uchovu.