China kuwasajili wafanyikazi upya

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption China kuwasajili wafanyikazi upya

Wakuu nchini China wametangaza mpango wa kuhalalisha ukaazi wa mamilioni ya wafanyakazi waliohamia mijini.

Mpango huu ukifanikiwa wafanyakazi hao wataweza kupata huduma, zikiwemo huduma za afya na elimu.

Kutoka mwezi ujao, wahamiaji hao waliotoka mashambani, wataweza kuomba haki ya ukaazi, katika miji sehemu zote za Uchina.

Ikiwa wameishi huko kwa angalau miezi sita, watahitajika kuthibitisha kuwa wana kibarua cha kutegemewa, au makaazi, au wanasoma.

Katika mpango wa sasa, wafanyakazi kutoka mashambani hawatambuliwi mijini, na watoto wao hawakubaliwi katika shule za serikali.

Kwa mujibu wa takwimu za benki ya dunia asilimia 70% ya wachina watakuwa wanaishi mijini kufikia mwaka wa 2030.

Haki miliki ya picha Xinhua
Image caption Aidha takwimu hiyo inasema takriban watoto milioni 61 hutelekezwa na wazazi wao ambao huhamia mijini.

Aidha takwimu hiyo inasema takriban watoto milioni 61 hutelekezwa na wazazi wao ambao huhamia mijini.

Sheria hizi mpya zitaanza kutekelezwa januari mosi.