Mkondo wa pili wa uchaguzi Ufaransa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wananchi wa Ufaransa wanapiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa serikali za majimbo

Wananchi wa Ufaransa wanapiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa serikali za majimbo, ambapo chama cha siasa kali za mrengo wa kulia, National Front, kinatarajiwa kupata wingi kwa mara ya kwanza katika angalu jimbo moja la nchi.

Chama kinachoongozwa na Bibi Marine Le Pen, kilipata kura nyingi kabisa katika duru ya kwanza juma lilopita.

Tangu wakati huo, chama tawala cha Socialist, kimejitoa katika sehemu kadha za nchi, ili wafuasi wake wakipigie kura chama cha mrengo wa kulia, cha Bwana Sarkozy, na hivyo wakishinde chama cha National Front.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kiongozi wa FN Marine Le Pen

Huu ndio uchaguzi mkubwa kabisa nchini Ufaransa, kabla ya uchaguzi wa rais wa mwaka 2017.

Chama hicho cha National Front kilipata asilimia 27.73% ya kura zote katika mkondo wa kwanza juma lililopita .

Chama cha aliyekuwa rais Sarkozy, Republican kilipata asilimia 26.65% ya kura huku chama cha rais wa sasa Francois Hollande cha Socialists kikimaliza katika nafasi ya tatu na asilimia 23.12%.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption National Front kilipata asilimia 27.73% Republican kinachoongozwa na Sarkozy kikimaliza katika nafasi ya pili na asilimia 26.65%

Kiongozi wa FN Marine Le Pen, anawania katika jimbo la kaskazini la Nord-Pas-de-Calais-Picardie.

Mwanaye bi Marion Marechal-Le Pen, anawania kuiwakilisha jimbo la Provence-Alpes-Cote d'Azur kusini mwa Ufaransa.

Wawili hao walishinda asilimia 40 % ya kura za mkondo wa kwanza.