Polisi 70 wajeruhiwa katika maandamano Ujerumani

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Meya wa mji wa Leipzig nchini Ujerumani ameeleza kushtuka kufuatia kujeruhiwa kwa maafisa wa polisi 70

Meya wa mji wa Leipzig nchini Ujerumani ameeleza kushtuka kufuatia kujeruhiwa kwa maafisa wa polisi 70 waliokabiliana na waandamanaji waliokuwa wakipinga wafasisti hiyo jana.

Meya Burkhard Jung, alisema kuwa waandamanaji wa mrengo wa kushoto walikuwa wakiwalenga hasa maafisa wa polisi katika mashambulizi yao.

Alisema kuwa vitendo vyao vilienda kinyume na kuhujumu yaliyopaswa kuwa maandamano ya amani ya kupinga makundi ya Kinazi mamboleo.

Waandamanaji wa mrengo wa kushoto walichoma mapipa ya uchafu na tairi na kutupa mawe, chupa na baruti za kujitengenezea katika juhudi za kuwazuia Wanazi mamboleo kuandamana.

Image caption Zaidi ya watu 20 walitiwa mbaroni.

Polisi kwa upande wao walitumia maji ya pilipili ya kutoa machozi .

Zaidi ya watu 20 walitiwa mbaroni.