Jeshi lazingira makao ya kiongozi Nigeria

Image caption Jeshi lazingira makao ya kiongozi Nigeria

Kundi moja la Waislamu Washia Kaskazini mwa Nigeria wanasema kuwa wanajeshi wamezingira makaazi ya kiongozi wao kufuatia mapigano ya jana ambapo watu kadhaa walifariki.

Kulingana na kundi la Islamic Movement of Nigeria, wanajeshi na vifaru vilitumika kushambulia makaazi ya Ibrahim Zakzaky katika mji wa Zaria, jimbo la Kaduna.

Kundi hilo lilisema wafuasi wake watano waliuawa.

Haki miliki ya picha
Image caption Wanajeshi na vifaru walitumika kushambulia makaazi ya Ibrahim Zakzaky mjini Zaria

Awali jeshi liliwalaumu mamia ya wafuasi wa kundi hilo la waislamu kwa kuzuia barabara moja na kufyatulia risasi msafara uliokuwa unambeba mkuu wa jeshi wa Nigeria.

Kundi hilo limakanusha madai hayo.