Mkataba wa tabia nchi waafikiwa Paris

Haki miliki ya picha AP
Image caption Huu ni mkataba wa kwanza wa kuwajibisha mataifa yote kupunguza ongezeko la hewa chafu duniani.

Mkataba umeafikiwa juu ya mabadiliko ya tabia nchi na mataifa karibu 200 katika mkutano wa viongozi wa mataifa uliofanywa mjini Paris, Ufaransa.

Wajumbe walishangilia na kukumbatiana wakati waziri wa mashauri ya kigeni wa Ufaransa, Laurent Fabius, aligonga kwenye meza kinyundo chake kuazimia kuwa mkataba umeafikiwa baada ya mashauriano ya majuma mawili.

Kulikuwepo na kushangilia, huku watu wamesimama kwa dakika kadhaa.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais Obama , amesema kuwa mkataba huo si kamilifu lakini unatoa nafasi bora zaidi ya kuokoa dunia.

Mkataba huo unanuia kupunguza kiwango cha joto duniani kwa nyuzijoto mbili .

Huu ni mkataba wa kwanza wa kuwajibisha mataifa yote kupunguza ongezeko la hewa chafu duniani.

Sehemu kadhaa za mkataba huo zinathibitisha kisheria lakini zingine zinatekelezwa kwa hiari.

Muda mfupi baada ya kuafikiwa mkataba huo wa tabia nchi, Rais Obama , amesema kuwa mkataba huo si kamilifu lakini unatoa nafasi bora zaidi ya kuokoa dunia.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Nayo Uchina, ambayo inatambuliwa, kama taifa linalochafua mazingira zaidi duniani, iliunga mkono mkataba huo

Alisema kuwa hiyo ni hatua muhimu inayoonyesha kuwa dunia ina nia na uwezo wa kukabiliana na changa moto ya kupunguza uchafuzi wa anga.

China, ambalo linatambuliwa kama taifa linalochafua dunia zaidi kwa hewa chafu, lilikaribisha mkataba huo lakini likasisitiza kuwa mataifa tajiri yanapaswa kutoa msaada wa kifedha kwa mataifa yanayostawi.

Kundi moja la wakereketwa, Global Justice Now, lililalamika kuwa halikushirikisha chochote kuhusiana na uwajibikaji wa mataifa kuhakikisha kuwa dunia patakuwa mahali salama na hali ya anga inayoweza kukalika na vizazi vijavyo.

Nayo Uchina, ambayo inatambuliwa, kama taifa linalochafua mazingira zaidi duniani, iliunga mkono mkataba huo na kusema kuwa umefungua njia ya kuimarisha zaidi juhudi za kupambana na mazingira mabovu.

Hata hivyo mjumbe wake, Shie Shenua, alisema kuwa mataifa tajiri lazima kuyasaidia kifedha mataifa yanayostawi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kulikuwepo na kushangilia, huku watu wamesimama kwa dakika kadhaa.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani, John Kerry, alisema mkataba huo ni ushindi kwa sayari ya dunia na kwa vizazi vijavyo kwa ujumla.

Jumuiya ya Ulaya ilipongeza Ufaransa kuwa kuyapatanisha mataifa ya dunia, muda mfupi tu baada ya mashambulizi ya Paris.

Mjumbe kutoka kisiwa cha St Lucia alisema kuwa mkataba huo utahakikisha kuwa kisiwa chake kina siku za usoni zenye matumiani bora zaidi.