ICTR kutoa hukumu ya mwisho leo

Image caption Baadhi ya majaji wa Mahakama ya ICTR Arusha Tanzania wakisikiliza moja kesi za mauaji ya Rwanda.

Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) iliyokuwa ikishughulikia kesi za mauaji yaliyotokea miaka 20 iliyopita leo itatoa hukumu yake ya mwisho kabla ya kufungwa kabisa.

Hukumu hiyo itakuwa dhidi ya watuhumiwa Pauline Nyiramasu ambaye ni waziri wa zamani wa Maendeleo ya wanawake nchini Rwanda na mtoto wake ambaye wote wamekana mashtaka yanayowakabili.

Mahakama hiyo ambayo imekuwako Kaskazini mwa Tanzania katika mji wa Arusha ilikuwa ikisikiliza kesi za watuhumiwa wa mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994.

Mara kadhaa waendesha mashtaka wa mahakama hiyo walikabiliwa na mashahidi waliokuwa tayari kutoa ushahidi.

Hata hivyo mafanikio yake yamepongezwa na watu wengi ambao wamesema si rahisi kuwatafuta na kushtaki watuhumiwa wote.