Sasa Bill Cosby awashtaki wanawake 40

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bill Cosby: Wanawake wananisingizia

Msanii wa Marekani Bill Cosby amewasilisha mashtaka ya kisheria akidai baadhi ya wanawake waliomshtaki walimsingizia wapate fedha

Amekuwa akishutumiwa kwa kuwanyanyasa kingono wanawake zaidi ya 40.

Bw Cosby mwenye umri wa miaka 78, amekanusha tuhuma dhidi yake na sasa amewashtaki wanawake hao wote akidai kuwa walikuwa na nia ya kumharibia jina na kufaidika kutokana na mali yake.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wakili wa wa wanawake hao bwana Joseph Cammarata,amesema kuwa hakuna shaka yeyote kuwa hatua ya Cosby ni hatua ya kulipiza kisasi.

Cosby anasema wamesababishia usumbufu mkubwa mno tangu waanze kujitokeza na tuhuma za uongo.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Amekuwa akishutumiwa kwa kuwanyanyasa kingono wanawake zaidi ya 40.

Aidha Cosby anasema wanawake hao wanamtupia dongo tu bila ushahidi wowote.

Msanii huyo nguli wa vichekesho, amechukua hatua hii baada ya wanawake 7 kuungana na kumshtaki kwa kuwadhulumu kimapenzi.

Wanawake hao kwa upande wao wanamshtaki Cosby kwa kujaribu kuwatupia tope tangu wajitokeze na madai hayo.

Hii ndio mara ya kwanza kwa wanawake hao kumfungulia Cosby Mashtaka.

Cosby amekiri na kukariri kuwa aliwahi kununua madawa na kuwashawishi wanawake hao kumeza kabla ya kushiriki ngono nao.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Bw Cosby amekanusha mashtaka hayo.

Cosby alitamba katika miaka ya themanini alipokuwa nyota wa kipindi cha vichekesho cha The Cosby Show.

The Cosby Show ilipendwa kote duniani kwa sababu ilikuwa ikiangazia maisha ya familia ya watu weusi raia wa Marekani.

Wakati huo alikuwa mwanaharakati mkubwa wa masomo haswa kwa jamii ya watu weusi.

Wakati madai haya yalipoibuka dhidi yake vyuo kadhaa vilivyokuwa vimemtambua na kumzawadi kwa mchango wake katika elimu ya watu weusi nchini Marekani walimvua mataji hayo huku makampuni mengi yakikata uhusiano naye.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mashirika ya utangazaji kama Netflix na NBC zilisimamisha mipango ya kupeperusha vipindi vyake vya runinga

Mashirika ya utangazaji kama Netflix na NBC zilisimamisha mipango ya kupeperusha vipindi vyake vya runinga

Wakili wa wa wanawake hao bwana Joseph Cammarata,amesema kuwa hakuna shaka yeyote kuwa hatua ya Cosby ni hatua ya kulipiza kisasi.

"ni vigumu sana kuamini kuwa wanawake hao wote walikutana na kupanga njama ya kumchafulia jina'' alisema bwana Cammarata.