Mourinho: Naona aibu

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Naona aibu baada ya kushindwa tena

Siku moja baada ya kuambulia kichapo cha 2-1 dhidi ya Leicester City , mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho sasa anadai wachezaji wanamsaliti

Mourinho anasema wamefanya kila jitihada katika mazoezi kuhakikisha kuwa the blues wanaibuka videdea lakini wapi !

''Inachosha sana kutizama kazi ambayo tumefanya ikisalitiwa'' alisema Mourinho.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mourinho anasema wamefanya kila jitihada katika mazoezi kuhakikisha kuwa the blues wanaibuka videdea lakini wapi !

''Moja ya vipawa vyangu tajika ni uwezo wa kusoma na kuelewa mchezo kwa haraka,,hii ndio nahisi nimesalitiwa''

''Wakati mwengine nahisi kama vile nilijitahidi kuimarisha uwezo wa wachezaji wetu msimu uliopita na sasa inaonekana wameshindwa kustahimili ushindani katika kiwango hicho''alifoka Mourinho.

Msimu uliopita Chelsea walipoteza katika mechi tatu tu walizoshiriki lakini msimu huu, mambo yamewageuka na maji yamezidi unga.

Chelsea walipoteza mechi yao ya 9 msimu huu kati ya 16 walizocheza.

The Blues sasa wamejipata katika nafasi ya 16 wakiwa na alama moja tu zaidi ya timu zinazotishiwa kushushwa daraja msimu ujao.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption The Blues sasa wamejipata katika nafasi ya 16 wakiwa na alama moja tu zaidi ya timu zinazotishiwa kushushwa daraja msimu ujao.

Hata hivyo kinachomkera sana raia huyo wa Ureno ni kichapo cha 2-1 mikononi mwa vinara wa ligi kuu ya Uingereza Leicester City.

Mabao ya Jamie Vardy na Riyad Mahrez yaliisaidia 'The Foxes' katika uwanja wao wa nyumbani wa King Power Stadium.

Kinachowashangaza wapenzi wa timu hiyo ni kwanini wachezaji walioishinda ligi msimu uliopita sasa wanashindwa hata kustahimili ushindani kutoka kwa timu ndogo.

Iwapo motisha katika timu ya Chelsea haitaimarika kwa haraka kuna hofu kibarua cha mreno huyo kitaingia mchanga.

Kocha huyo wa Chelsea anakila sababu ya kuwa na hofu haswa wakijiandaa kukabiliana na Sunderland siku ya jumamosi.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kocha huyo wa Chelsea anakila sababu ya kuwa na hofu haswa wakijiandaa kukabiliana na Sunderland siku ya jumamosi.

Mourinho amekiri kuwa sasa haitawezekana kwa the Blues kufuzu kwa kinyang'anyiro cha kuwania kombe la mabingwa barani ulaya mwakani.

''Hatuwezi maliza katika nafasi 4 za kwanza ila tukijitahidi huenda tukacheza katika ligi ya Europa'' alisema Mourinho.

'Naona haya bila shaka'