Sudan Kusini kukosa chakula

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mapigano nchini Sudani kusini yamesabisha maelfu ya Watu kukimbia makazi yao

Miaka miwili tangu machafuko yalipoanza Sudan kusini, mashirika ya misaada wanatahadharisha kuhusu upungufu mkubwa wa chakula kukumba nchi hiyo na kutaka hatua zichukuliwe kumaliza vitendo vya uhalifu wa kivita ndani ya taifa hilo changa.

Ingawa makubaliano ya amani yalitiwa saini miezi kadhaa iliyopita, machafuko bado yanaendelea na karibu watu milioni moja na nusu wamelazimika kuyahama makazi yao.

Idadi hii inashtusha.

Karibu watu milioni nne hawana chakula, kama Umoja wa mataifa ulivyoeleza ambapo idadi hiyo ni takriban theluthi moja ya idadi ya watu wa Sudani Kusini.

Watu elfu thelathini wanakabiliwa na njaa kali, na wakati mapigano yanapoendelea na mvua zinazonyesha kwa uchache mwaka huu hali ni inaendelea kuwa mbaya.

Tangu kuanza kwa mapigano nchi nzima miaka miwili iliyopita, Rais na makamu wa rais wa zamani wa nchi hiyo wameshindwa kutekeleza makubaliano ya kuleta amani.

Mapigano yamelazimu watu 185,000 kutafuta hifadhi kwenye kambi za Umoja wa mataifa.

Hali hii ya imesababisha kusambaa kwa maradhi, utapiamlo, pia kumekuwa na matukio mengi ya mauaji, ubakaji na uhalifu mwingine wa kivita.