Serikali, FARC kumaliza mzozo wa Colombia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mzozo wa Colombia umegharimu maelfu ya maisha ya Watu

Rais wa Colombia, Juan Manuel Santos amesema makubaliano yaliyofikiwa kati ya Serikali na waasi wa FARC ni hatua kubwa katika juhudi za kufanikisha kutiwa saini kwa mkataba wa amani mwezi Machi mwakani.

Akihutubia kwa njia ya televisheni, Rais Santos amesema pande hizo mbili zimeafikiana katika mambo manne kati ya matano.

Makubaliano haya ya sasa yanawaweka waathirika wa mzozo wa nchini humo katika hali ya matumaini ya kufikiwa kwa mchakato wa amani.

Watu takriban 200,000 wamepoteza maisha kutokana na mzozo na wengine milioni sita wanakadiriwa kuyakimbia makazi yao.