Eto’o apewa kazi ya ukufunzi Uturuki

Eto'o Haki miliki ya picha AFP
Image caption Eto'o alistaafu soka ya kimataifa mwaka uliopita

Nyota wa zamani wa Barcelona, Inter Milan na Chelsea Samuel Eto’o ameteuliwa kuwa kaimu mkufunzi wa klabu ya Antalyaspor ya Uturuki.

Eto’o atasaidiana na mkufunzi wa timu ya vijana ambaye pia ni mkurugenzi wa ufundi Mehmet Ugurlu.

Atapewa kazi hiyo kwa mkataba wa muda mrefu iwapo klabu hiyo itafanya vyema kwenye mechi tatu kabla ya mapumziko mafupi ya majira ya baridi.

Eto’o alijiunga na Antalyaspor kama mchezaji 25 Juni kwa mkataba wa miaka mitatu na akawachezea mechi ya kwanza ligini Agosti 2015 dhidi ya Istanbul Basaksehir.

Alifunga mabao mawili mechi hiyo na kuwasaidia kushinda 3-2.

Eto’o, mwenye umri wa miaka 34 aliacha kuchezea timu ya taifa ya Cameroon mwaka jana.

Amepewa majukumu hayo mapya baada ya kufutwa kazi kwa kocha Simsek.