Miili ya watu 19 yagunduliwa Mexico

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Polisi wakilinda miili ya watu iliyogunduliwa Mexico.

Miili ya watu wapatao 19 imepatikana katika jimbo la Mexico la Guerrero, ambako wanafunzi 43 walitoweka mwaka jana.

Polisi wanasema miili hiyo ilitupwa kwenye mto mwembamba, wenye kina cha mita mia tano katikati ya miamba na miti karibu na kijiji cha Chichi-hua-lco.

Miili nane kati ya hiyo ilikuwa inaonekana kuchomwa baadhi ya viungo.

Vipimo vya DNA vinatarajiwa kuchukuliwa kutoka katika familia za wanafunzi hao waliokufa, kuweza kujua kama ni kweli ni hao, ambao hawajapatikana mpaka sasa.