Pakistan yakumbuka shambulio lililoua 150

Pakistan Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waziri mkuu wa Pakistan amesema shambulio hilo "lilitikisa taifa"

Ibada imeandaliwa kuwakumbuka watu 150 waliouawa katika shule moja eneo la Peshawar, Pakistan mwaka mmoja uliopita.

Waziri mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif, ameambia waliohudhuria kwamba shambulio hilo la Taliban katika shule ya umma ya jeshi “lilitikisa taifa”.

Walimu na wanafunzi wamesimulia kuhusu waliovyoathiriwa na shambulio hilo.

Baadhi ya wanafunzi wamesema bado wanahitaji usaidizi wa kimatibabu na kisaikolojia.

Katika mji wa Lahore, magari yamesimamishwa katika taa za barabarani kwa dakika mbili.

Katika kituo cha runinga cha Geo, watangazaji wamevalia sare za wanafunzi wa shule iliyoshambuliwa kuonyesha hisia zao.