Ripoti mpya ya UNICEF yashtua

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Miongoni mwa watoto wanaozaliwa katika maeneo yenye vita wakiwa na mama zao.

Zaidi ya watoto milioni 16 duniani, wamezaliwa katika mazingira ya kivita katika kipindi cha mwaka mmoja pekee.

Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa mataifa linaloshugulikia maswala ya watoto UNICEF imesema kila baada ya sekunde mbili mtoto mmoja huzaliwa katikati ya mizozo ya kivita.

Ripoti hiyo inasema pia katika maeneo hayo hakuna huduma za afya.

Idadi ya watu wasio na makao imeongezeka maradufu tangu vita vya pili vya dunia.