Akamatwa akihusishwa na mauaji California

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mashambulizi ya mjini California yaligharimu maisha ya watu 14

Rafiki wa wapenzi waliotekeleza mashambulizi na kusababisha mauaji ya watu 14 mjini San Bernardino huko California nchini Marekani mwanzoni mwa mwezi huu amekamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya kushirikiana kufanya kosa la ugaidi.

Enriquez Marquez anashutumiwa kununua silaha mbili kinyume cha sheria ambazo zilitumika na Syed Rizwan Farok na Mkewe Tashfeen Malik pia alinunua malighafi iliyotumika kutengeneza Bomu.

Marquez amekana mashtaka akisema kuwa hakufahamu mipango ya wapenzi hao.

Mtu mwingine Jalil bin Ameer Aziz amekamatwa pennyslvania kwa kosa la kushiriki na kujaribu kutoa msaada wa mali kwa kundi la Islamic state

wapelelezi wanasema Enriquez alibadili dini na kuwa muislamu baada ya kufahamiana na jirani yake Syed Rizwan Farook.

Inaelezwa kuwa walikuwa wakitazama picha za video zinazohusiana na maswala ya itikadi kali za kiislamu na walipanga mipango ya mashambulizi ya kigaidi mwaka 2011 na 2012 huko califonia.

Maafisa upelelezi wanasema kuwa wapenzi walipanga kurusha mabomu katika mgahawa wa wanafunzi kabla ya kufanya mashambulizi kwa risasi . Pia walipanga mipango ya kushambulia abiria wakiwa kwenye magari wakati wa muda wa pilika nyingi.

Enriquez mwenye umri wa miaka 24 anatuhumiwa pia kwa udanganyifu kuingia kwenye ndoa ya udanganyifu na mmoja wa mwanafamilia wa Farook.kwa makosa matatu yanayomkabili iwapo atakutwa na hatia atahukumiwa kifungo cha jumla ya miaka 35 gerezani.