Mamilioni ya dola kwa picha za Marais

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Picha za Rais Mahama na watangulizi wake zinadaiwa kutumia karibu dola milioni moja

Kumekua na ghadhabu ya umma nchini Ghana baada ya serikali kutumia karibu dola milioni moja kubandika picha za Marais wa nchi hiyo kwenye mabasi ya uchukuzi wa umma.

Zaidi ya magari 100 yamebandikwa picha za Rais wa sasa John Mahama na watangulizi wake. Ghana inakumbwa na msukosuko wa kiuchumi kiasi cha kulazimika kutoa umeme kwa mgao.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Picha za Rais Mahama na watangulizi wake zimebandikwa kwenye mabasi ya umma

Kumekua na madai ya ufisadi serikalini katika miezi ya karibuni.Raia wengi wanasema fedha hizo zimengetumika kwenye huduma muhimu.

Aidha kuna lalama kwamba picha za Rais Mahama zinatumika kama kampeini yake kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka ujao.