Wanyarwanda waidhinisha marekebisho ya katiba

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kagame amekuwa rais tangu 2000

Wanyarwanda wameunga mkono kwa wingi marekebisho ya katiba ambayo yatamruhusu Rais Paul Kagame kuendelea kuongoza, matokeo ya awali ya kura ya maoni yanaonyesha.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inasema 98% ya wapiga kura wameunga mkono marekebisho hayo ya katiba ambayo yatamruhusu Bw Kagame kuwania kwa muhula mwingine mwaka 2017, baada yake kumaliza muhula wa pili.

Tume hiyo imesema wilaya 21 kati ya wilaya 30 zimechapisha matokeo yake kufikia sasa.

Matokeo kamili yatatolewa baadaye leo Jumamosi.

Bw Kagame, 58, huenda akaongoza hadi 2034 iwapo marekebisho hayo yataidhinishwa.

Kura hiyo ilipigwa licha ya kukosolewa na Marekani na mataifa mengine kutoka Magharibi.

Image caption Kagame bado hajatangaza iwapo atawania urais tena

Bw Kagame bado hajatangaza iwapo atawania tena, ingawa wengi wanatarajia afanye hivyo.

Kiongozi huyo amekuwa rais tangu 2000 lakini alikuwa na mamlaka tangu 1994 wapiganaji wa kundi lake walipoingia mji mkuu Kigali kusitisha mauaji ya kibali.

Mjadala kuhusu kuongezwa kwa mihula ya rais umesababisha vurugu katika nchi nyingine za Afrika kama vile Burundi na Jamhuri ya Congo, lakini vurugu hazitajokea Rwanda.