Air France: 'Bomu' ilikuwa bandia

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Air France: 'Bomu' ilikuwa ya uongo

Mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege la Air France amefutilia mbali tahadhari ya bomu iliyosababisha ndege ya kutua Kenya kuwa ni ya uongo

Frederic Gagey amewaambia waandishi wa habari mjini Paris Ufaransa kuwa kifaa kilichodhaniwa kuwa kilipuzi kilikuwa ni mbao na kisanduku cha karatasi tu wala haikuwa na hatari yeyote kwa usalama wa ndege hiyo.

Haki miliki ya picha Karim Rajan
Image caption Ndege hiyo ilikuwa na abiria 459 na wahudumu 14.

Mhudumu huyo alimfahamisha rubani kuhusiana na kifaa hicho na shughuli za kutua kwa dharura zikaanza.

Ndege hiyo ilikuwa na abiria 459 na wahudumu 14.

Ndege hiyo ilitua saa sita usiku wa kuamkia leo Jumapili, huku wataalamu wa kutegua mabomu kutoka jeshi la wanamaji la Kenya wakiingia ndani ya ndege hiyo kukagua kifurushi kilicholeta taharuki.

Sasa kitengo cha ujasusi cha Ufaransa kimeanzisha uchunguzi wa kina kubaini kilichosababisha tishio hilo.