Majengo 22 yaporomoka China

Haki miliki ya picha Shenzhen Municipal Public Security Fire Brigade
Image caption Majengo 22 yaporomoka China

Majengo 22 yameporomoka katika maeneo ya viwandani katika mji wa Shenzhen, Kusini mwa Uchina kufuatia maporomoko ya ardhi.

Takriban watu 900 waliokolewa kabla ya maporomoko hayo kutokea.

Hata hivyo waokoaji wanaendelea kuwatafuta watu ambao wanashukiwa kuwa wamekwama ndani ya vifusi vya majengo hayo yaliyoporomoka

Hadi kufikia sasa hakuna mtu aliyeripotiwa kufarika ijapokuwa watu 22 hawajulikani waliko.

Mbili kati ya majumba hayo yalikuwa nyumba za malazi za wafanyikazi wa ujenzi na yamkini watu wanne wametolewa ndani ya vifusi vya majengo yaliyoanguka.

Haki miliki ya picha Xinhua
Image caption Wazima moto 1,500 wanaendelea na shughuli ya uokoaji.

Naibu mwenyekiti wa mji huo Li Yikang, amesema wanawake 5 na wanaume 17 hawajulikani waliko.

Wazima moto 1,500 wanaendelea na shughuli ya uokoaji.

Kulingana na vyombo vya habari mchanga ambao umekuwa ukichimbwa kwa muda wa miaka miwili unaaminika kuwa ulilowa na kuporomoka.