Aliyebaka na kuua achiwa huru nchini India

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Aliyebaka na kuua achiwa huru nchini India

Mfungwa mchanga zaidi katika genge la wabakaji waliopatikana na hatia ya kubaka na kuua mwanamke mmoja mwaka wa 2012 ameachiwa huru.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wakili wake amaeithibitishia shirika la BBC kuwa kijana huyo ambaye alihukumiwa akiwa chini ya umri wa miaka 18 alifungwa kwa miaka 3 ambayo inaruhusiwa kisheria.

Wakili wake amaeithibitishia shirika la BBC kuwa kijana huyo ambaye alihukumiwa akiwa chini ya umri wa miaka 18 alifungwa kwa miaka 3 ambayo inaruhusiwa kisheria.

Japo hivi sasa ametimiza miaka 18 ameruhusiwa kuachiwa huru kisheria na kupewa majina mapya na hata makosa yaliyomkabili yamefutwa.

Kijana huyo ambaye hawezi tajwa ameondoka gerezani fauka ya pingamizi kutoka kwa mashirika ya wanaharakati wa maswala ya wanawake na wazazi wa mhasiriwa wa ubakaji huo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mamake msichana aliyebakwa hadi kufariki alikamatwa katika maandamano mjini Delhi

Kwa sasa amekabidhiwa shirika linalowashughulikia wafungwa ambao hawajatimiza umri wa utu uzima kutokana na hofu kuhusu usalama wake.

Wanne kati ya watuhumiwa waliotenda makosa hayo naye wamekata rufaa huku mtuhumiwa wa tano akiripotiwa kufariki akiwa gerezani.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanne kati ya watuhumiwa waliotenda makosa hayo naye wamekata rufaa

Mwandishi wa BBC Sanjoy Majumder aliyeko Delhi anasema kuwa wanaharakati wengi wamejaribu kuzuia kuachiliwa huru kwa mtuhumiwa huyo japo mahakama inasisistiza kuwa inafwata sheria.

Wazazi wa mhasiriwa ambaye kifo chake kilisababisha ghadhabu kote duniani wanapinga kuachiliwa huru kwa kijana huyo.