Syria yashambulia ngome za waasi

Maelfu ya watu wameuawa upande wa kaskazini-magharibi mwa Syria katika mfululizo wa mashambulizi ya anga yaliyotokea katika mji wa Idlib.wakaazi wa mji huo wamesema kwamba eneo la soko, makaazi ya watu, na majengo kadhaa yamegongwa .

Lakini kikundi kinachofuatilia mzozo huo, waangalizi wa haki za binaadamu nchini Syria, wameeleza kuwa shambulio hilo lililenga zaidi maeneo yanayoshikiliwa na waasi na wengi wa waliokufa walikuwa wapiganaji waliovalia sare za kijeshi .

Nao wenyeji wa mji huo wameeleza kuwa mashambulizi hayo ya anga yamefanywa na ndege za kivita za majeshi ya Urusi,ingawa mpaka sasa Urusi yenyewe haijathibitisha juu ya suala hilo.

Kwingineko,runinga ya taifa la Syria imetoa taarifa kuwa watu kumi wamejeruhiwa wakiwa katika basi la jeshi katika mji mkuu wa nchi hiyo , Damascus.