Wito wa kusitishwa kwa mauaji ya Burundi ukiwa umeandikwa kwenye bango , lililotelekezwa barabarani
Huwezi kusikiliza tena

Burundi halihitaji jeshi la AU

Wabunge nchini Burundi wameanza mjadala kuhusu hatua ya muungano ya Afrika wa kutuma kikosi cha wanajeshi wapatao 5000 cha kulinda amani nchini humo, hatua ambayo inafaa kuidhinishwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.Hatua hiyo imepingwa vikali na serikali ya rais Pierre Nkurunziza, ikitaja kikosi hicho kuwa cha kigeni kinachovamia taifa hilo.

Kufuatia msimamo wa bunge la nchi hiyo kukataa majeshi ya muungano huo, mwandishi wa BBC Regina Mziwanda alizungumza na mchambuzi wa masuala ya kisiasa wa eneo la maziwa Makuu bwana Khalid Hassan kutaka kujua masuala kadhaa kuhusiana na uamuzi wa bunge hilo na mustakabali wa Burundi.